caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 155

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:155

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوْا۟ مِنكُمْ يَوْمَ ٱلْتَقَى ٱلْجَمْعَانِ إِنَّمَا ٱسْتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا۟ وَلَقَدْ عَفَا ٱللَّهُ عَنْهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, wale waliogeuka wakakimbia miongoni mwenu siku yalipokutana makundi mawili, hakika Shetani tu ndiye aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyoyafanya. Na Mwenyezi Mungu amekwishawasamehe. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika wale walio rudi nyuma miongoni mwenu siku yalipo pambana majeshi mawili, Shet'ani ndiye aliye watelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyo yafanya; na Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70