إِذْ تُصْعِدُونَ وَلَا تَلْوُۥنَ عَلَىٰٓ أَحَدٍ وَٱلرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ فِىٓ أُخْرَىٰكُمْ فَأَثَٰبَكُمْ غَمًّۢا بِغَمٍّ لِّكَيْلَا تَحْزَنُوا۟ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا مَآ أَصَٰبَكُمْ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterPale mlipokuwa mkikimbia mbio, wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anawaita, yuko nyuma yenu. Basi Mwenyezi Mungu akawapa dhiki juu ya dhiki, ili msisikitike kwa yale yaliyowakosa wala kwa yale yaliyowapata. Na Mwenyezi Mungu ana habari za yote mnayoyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniPale mlipo kuwa mkikimbia mbio wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anakuiteni, yuko nyuma yenu. Mwenyezi Mungu akakupeni dhiki juu ya dhiki, ili msisikitike kwa yaliyo kukoseeni wala kwa yaliyo kusibuni. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.