caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 152

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:152

وَلَقَدْ صَدَقَكُمُ ٱللَّهُ وَعْدَهُۥٓ إِذْ تَحُسُّونَهُم بِإِذْنِهِۦ حَتَّىٰٓ إِذَا فَشِلْتُمْ وَتَنَٰزَعْتُمْ فِى ٱلْأَمْرِ وَعَصَيْتُم مِّنۢ بَعْدِ مَآ أَرَىٰكُم مَّا تُحِبُّونَ مِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلدُّنْيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلْـَٔاخِرَةَ ثُمَّ صَرَفَكُمْ عَنْهُمْ لِيَبْتَلِيَكُمْ وَلَقَدْ عَفَا عَنكُمْ وَٱللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu aliwatimilizia ahadi yake, vile mlivyokuwa mnawaua kwa idhini yake, mpaka mlipolegea na mkazozana katika amri hii, na mkaasi baada ya Yeye kuwaonyesha yale mnayoyapenda. Wapo miongoni mwenu wanaotaka dunia, na wapo miongoni mwenu wanaotaka Akhera. Kisha akawatenga nao (maadui) ili akujaribuni. Naye sasa amekwishawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu alikutimilizieni miadi yake, vile mlivyo kuwa mnawauwa kwa idhini yake, mpaka mlipo legea na mkazozana juu ya amri, na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni mliyo yapenda. Wapo miongoni mwenu wanao taka dunia, na wapo miongoni mwenu wanao taka Akhera. Kisha akakutengeni nao (maadui) ili akujaribuni. Naye sasa amekwisha kusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70