caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 60

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:60

وَإِذِ ٱسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ فَقُلْنَا ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْحَجَرَ فَٱنفَجَرَتْ مِنْهُ ٱثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ مِن رِّزْقِ ٱللَّهِ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa alipoomba maji kwa ajili ya watu wake, tukamwambia: 'Lipige jiwe kwa fimbo yako.' Mara zikatimbuka chemichemi kumi na mbili; kila kabila likajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe katika riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70