caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Hadid, Aya 14

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 94 · 57:14

يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ قَالُوا۟ بَلَىٰ وَلَٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَٱرْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ ٱلْأَمَانِىُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمْرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلْغَرُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatawaita wawaambie: 'Kwani hatukuwa pamoja nanyi?' Watawaambia: 'Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya (Waumini), na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu yule[1] akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWatawaita wawaambie: Kwani vile hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkasitasita, na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni. mpaka ilipo kuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70