caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 97

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:97

جَعَلَ ٱللَّهُ ٱلْكَعْبَةَ ٱلْبَيْتَ ٱلْحَرَامَ قِيَٰمًا لِّلنَّاسِ وَٱلشَّهْرَ ٱلْحَرَامَ وَٱلْهَدْىَ وَٱلْقَلَٰٓئِدَ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَأَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ameifanya Al-Kaaba, hii Nyumba Tukufu, kuwa ya kuwakimu watu, na Miezi Mitakatifu, na dhabihu walioletwa Makka kama zawadi, na dhabihu waliofungwa vigwe. Hayo ni ili mjue ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika mbingu na yaliyo katika ardhi, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu ameifanya Al Kaaba, hii Nyumba Tukufu, ni simamio la watu, na kadhaalika Miezi Mitukufu, na wanyama wa dhabihu, na vigwe. Hayo ili mjue ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo katika ardhi, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70