إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِىٓ أَنفُسِهِمْ قَالُوا۟ فِيمَ كُنتُمْ قَالُوا۟ كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِى ٱلْأَرْضِ قَالُوٓا۟ أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةً فَتُهَاجِرُوا۟ فِيهَا فَأُو۟لَٰٓئِكَ مَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ وَسَآءَتْ مَصِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, wale ambao Malaika wanawafisha hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao, watawaambia: 'Mlikuwa katika nini?' Watasema: 'Tulikuwa tumefanywa kuwa wanyoge katika ardhi.' Watawaambia: 'Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa, mkahamie humo?' Basi hao makazi yao ni Jahannam, nayo ni marejeo mabaya kabisa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa.