caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 155

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:155

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَٰقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَقَتْلِهِمُ ٱلْأَنۢبِيَآءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌۢ بَلْ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kwa sababu ya kuvunja kwao maagano yao, na kuzikufuru kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: 'Nyoyo zetu zimefumbwa'; bali Mwenyezi Mungu ameziziba kwa kufuru zao, basi hawaamini isipokuwa kidogo tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi zao, na kuzikataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri kwa kufuru zao, basi hawaamini ila kidogo tu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70