caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 135

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:135

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوا۟ قَوَّٰمِينَ بِٱلْقِسْطِ شُهَدَآءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمْ أَوِ ٱلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَٱللَّهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا فَلَا تَتَّبِعُوا۟ ٱلْهَوَىٰٓ أَن تَعْدِلُوا۟ وَإِن تَلْوُۥٓا۟ أَوْ تُعْرِضُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Kuweni wenye kusimama imara katika kufanya uadilifu, wenye kushuhudia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hata kama ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au fukara, Mwenyezi Mungu ndiye anayewastahiki zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkaupa mgongo, basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayoyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70