caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 73

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:73

وَلَا تُؤْمِنُوٓا۟ إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ ٱلْهُدَىٰ هُدَى ٱللَّهِ أَن يُؤْتَىٰٓ أَحَدٌ مِّثْلَ مَآ أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَآجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ قُلْ إِنَّ ٱلْفَضْلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msimuamini isipokuwa yule anayeifuata dini yenu. Sema: Hakika uongofu ni uongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa yale mliyopewa nyinyi au wawahoji mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa hizo amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa mlio pewa nyinyi au wakuhojini mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70