caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 220

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:220

فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَيَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْيَتَٰمَىٰ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَٰنُكُمْ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ ٱلْمُفْسِدَ مِنَ ٱلْمُصْلِحِ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَعْنَتَكُمْ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika dunia na Akhera, na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio heri. Na mkichanganyika nao, basi ni ndugu zenu. Na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angelipenda, angelikutieni katika ugumu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani--Katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera. Na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio kheri. Na mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu; na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angeli penda angeli kutieni katika udhia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70