إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلْكِتَٰبِ وَيَشْتَرُونَ بِهِۦ ثَمَنًا قَلِيلًا أُو۟لَٰٓئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِى بُطُونِهِمْ إِلَّا ٱلنَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, na wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali katika tumbo zao isipokuwa moto. Wala Mwenyezi Mungu hatawaongelesha Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao wana adhabu chungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipo kuwa moto, wala Mwenyezi Mungu hatawasemeza Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Nao watapata adhabu chungu.