لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَٰقَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ وَأَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمْ رُسُلًا كُلَّمَا جَآءَهُمْ رَسُولٌۢ بِمَا لَا تَهْوَىٰٓ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا۟ وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, tulichukua agano la Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipowajia Mtume kwa yale zisiyoyapenda nafsi zao, wengine wao waliwakanusha, na wengine wao wakawaua.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniTulifanya agano na Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipo wajia Mtume kwa wasio yapenda nafsi zao wengine waliwakanusha na wengine wakawauwa.