caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 69

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:69

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلصَّٰبِـُٔونَ وَٱلنَّصَٰرَىٰ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale walioamini, na Mayahudi, na Masabii na Wakristo, mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi hawatakuwa na hofu juu yao wala hawatahuzunika.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70