caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 66

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:66

وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا۟ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَآءَ مَا يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa wangeliisimamisha Taurati na Injili na yote waliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wao Mlezi, basi hakuna shaka wangelikula kutokea juu yao na kutokea chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70