وَقَفَّيْنَا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم بِعِيسَى ٱبْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَءَاتَيْنَٰهُ ٱلْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawafuatishia nyuma yao, Isa mwana wa Maryam akiyasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyo na uongofu ndani yake, na ni nuru, na inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na ni uwongofu na mawaidha kwa wacha Mungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu.