وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ٱبْنَىْ ءَادَمَ بِٱلْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ ٱلْـَٔاخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلْمُتَّقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasomee habari za wana wawili wa Adam kwa haki. Walipotoa mhanga, basi ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwingine haukukubaliwa. Akasema (yule ambaye haukukubaliwa mhanga wake): Lazima nitakuua. Akasema huyo mwingine: Hakika Mwenyezi Mungu hupokea tu kutoka kwa wacha Mungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu.