يَٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَٰبِ قَدْ جَآءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ ٱلْكِتَٰبِ وَيَعْفُوا۟ عَن كَثِيرٍ قَدْ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٌ وَكِتَٰبٌ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi Watu wa Kitabu! Hakika amekwishawajia Mtume wetu anayewabainishia mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anayaacha mengi. Bila shaka imekwishawajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kilicho wazi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha.