لَّٰكِنِ ٱلرَّٰسِخُونَ فِى ٱلْعِلْمِ مِنْهُمْ وَٱلْمُؤْمِنُونَ يُؤْمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَٱلْمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱلْمُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلْمُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ أُو۟لَٰٓئِكَ سَنُؤْتِيهِمْ أَجْرًا عَظِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini waliobobea katika elimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini yale yaliyoteremshwa juu yako, na yale yaliyoteremshwa kabla yako. Na wanaosimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, hao tutawapa malipo makubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniLakini walio bobea katika ilimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini uliyo teremshiwa wewe, na yaliyo teremshwa kabla yako. Na wanao shika Swala, na wakatoa Zaka, na wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho - hao tutawapa malipo makubwa.