إِنَّآ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ كَمَآ أَوْحَيْنَآ إِلَىٰ نُوحٍ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعْدِهِۦ وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْمَٰعِيلَ وَإِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيْمَٰنَ وَءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ زَبُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tumekufunulia ufunuo (wahyi) wewe kama tulivyomfunulia ufunuo (wahyi) Nuhu na Manabii waliokuwa baada yake. Na tulimfunulia ufunuo (wahyi) Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wanawe, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, naye Daud tukampa Zaburi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.