caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 119

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:119

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَـَٔامُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ ءَاذَانَ ٱلْأَنْعَٰمِ وَلَـَٔامُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ ٱللَّهِ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيْطَٰنَ وَلِيًّا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika nitawapoteza, na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi hakika watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi hakika watabadili aliyoumba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shetani kuwa ni rafiki mwandani badala ya Mwenyezi Mungu, basi hakika amehasiri hasara ya dhahiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70