بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَآءً وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِى تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلْأَرْحَامَ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi ambaye aliwaumba kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka kwayo. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaomba, na jamaa zenu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalia.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.