وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُۥنَ أَلْسِنَتَهُم بِٱلْكِتَٰبِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ ٱلْكِتَٰبِ وَمَا هُوَ مِنَ ٱلْكِتَٰبِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika wapo miongoni mwao kundi lipindualo ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhani kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Nao husema: 'Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu.' Na wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wanasema uongo juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wapo baadhi yao wanao pindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na wao wanajua.