إِذْ قَالَتِ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ يَٰمَرْيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ ٱسْمُهُ ٱلْمَسِيحُ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَمِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterPale Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika, Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya (mwana kwa) neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryam, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na ni miongoni mwa waliowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu).
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).