فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّى وَضَعْتُهَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلْأُنثَىٰ وَإِنِّى سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّىٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيْطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipomzaa, akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, nimemzaa wa kike - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa. Na wa kiume si sawa na wa kike. Na mimi kwa hakika nimemwita Mariam. Nami kwa hakika ninamkinga kwako, yeye na dhuria yake kutokana na Shetani aliyelaaniwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet'ani aliye laaniwa.