وَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ نَافَقُوا۟ وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ قَٰتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوِ ٱدْفَعُوا۟ قَالُوا۟ لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَّٱتَّبَعْنَٰكُمْ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَٰنِ يَقُولُونَ بِأَفْوَٰهِهِم مَّا لَيْسَ فِى قُلُوبِهِمْ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ili awajue wale waliofanya unafiki, walipoambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: 'Tungelijua kuna kupigana vita, bila ya shaka tungeliwafuata.' Wao siku ile walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyaficha.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ili awapambanue walio kuwa wanaafiki, wakaambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: Tungeli jua kuna kupigana bila ya shaka tungeli kufuateni. Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyo kuwamo nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua kabisa wanayo yaficha.