caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 112

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:112

ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ ٱلذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوٓا۟ إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَحَبْلٍ مِّنَ ٱلنَّاسِ وَبَآءُو بِغَضَبٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ ٱلْمَسْكَنَةُ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقْتُلُونَ ٱلْأَنۢبِيَآءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا۟ وَّكَانُوا۟ يَعْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUmepigwa udhalilifu juu yao popote wanapokutwa, isipokuwa kwa kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na walirudi na ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na unyonge umepigwa juu yao. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwaua Manabii bila ya haki. Hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wamepigwa na unyonge. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasina haki; hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70