وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ ءَايَةَ مُلْكِهِۦٓ أَن يَأْتِيَكُمُ ٱلتَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ ءَالُ مُوسَىٰ وَءَالُ هَٰرُونَ تَحْمِلُهُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Nabii wao akawaambia: Hakika, alama ya ufalme wake ni kwamba awaletee lile sanduku ambalo ndani yake mna kituliza nyoyo zenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na mabaki ya waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Harun, linalobebwa na Malaika. Bila shaka, katika hayo zimo ishara kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni kukuleteeni lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza nyoyo zenu, kitokacho kwa Mola wenu Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina Harun, wanalichukua Malaika. Bila shaka katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini.