caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 213

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:213

كَانَ ٱلنَّاسُ أُمَّةً وَٰحِدَةً فَبَعَثَ ٱللَّهُ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ ٱلْكِتَٰبَ بِٱلْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ ٱلنَّاسِ فِيمَا ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ وَمَا ٱخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ أُوتُوهُ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَٰتُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ فَهَدَى ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لِمَا ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ مِنَ ٱلْحَقِّ بِإِذْنِهِۦ وَٱللَّهُ يَهْدِى مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatu wote walikuwa umma mmoja. Kisha Mwenyezi Mungu akawatuma Manabii wenye kupeana habari njema na waonyaji. Na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitilafiana. Na wala hawakuhitilafiana ndani yake isipokuwa wale waliopewa Kitabu hicho baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi, kwa sababu ya husuda ya baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walioamini kuiendea haki katika yale waliyohitilafiana ndani yake. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWatu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walio amini kwendea haki katika mambo waliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70