caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 191

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:191

وَٱقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ وَٱلْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلْقَتْلِ وَلَا تُقَٰتِلُوهُمْ عِندَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَٰتِلُوكُمْ فِيهِ فَإِن قَٰتَلُوكُمْ فَٱقْتُلُوهُمْ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waueni popote muwakutapo, na watoeni popote walipowatoa; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wawapigie huko. Wakikupigeni huko, basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70