إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَآ أَنزَلْنَا مِنَ ٱلْبَيِّنَٰتِ وَٱلْهُدَىٰ مِنۢ بَعْدِ مَا بَيَّنَّٰهُ لِلنَّاسِ فِى ٱلْكِتَٰبِ أُو۟لَٰٓئِكَ يَلْعَنُهُمُ ٱللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ ٱللَّٰعِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, wale wanaoficha yale tuliyoyateremsha, nazo ni hoja zilizo wazi na uongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.