caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 158

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:158

إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلْمَرْوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِ فَمَنْ حَجَّ ٱلْبَيْتَ أَوِ ٱعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ ٱللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi, anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuzunguka kati yake. Na anayejitolea kutenda heri, basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mwenye kujua hilo mno.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anaye hiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anaye jitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mjuzi.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70