وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا ٱسْمُهُۥ وَسَعَىٰ فِى خَرَابِهَآ أُو۟لَٰٓئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَآ إِلَّا خَآئِفِينَ لَهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا خِزْىٌ وَلَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake, na akajitahidi kuiharibu? (Watu) hao haitawafalia kuingia humo isipokuwa kwa hofu. Duniani watapata hizaya (aibu kubwa maishani), na Akhera watapata adhabu kubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa.