لَيْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوٓا۟ إِذَا مَا ٱتَّقَوا۟ وَّءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ ثُمَّ ٱتَّقَوا۟ وَّءَامَنُوا۟ ثُمَّ ٱتَّقَوا۟ وَّأَحْسَنُوا۟ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakuna ubaya juu ya wale walioamini na wakatenda mema kwa vile walivyovila (zamani) maadamu wakimcha Mungu na wakiamini na wakitenda mema, kisha wakamcha Mungu, na wakaamini, kisha wakamcha Mungu na wakafanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mazuri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSi dhambi juu ya walio amini na wakatenda mema kwa walivyo vila (zamani) maadamu wakichamngu na wakiamini na wakitenda mema, kisha wakachamngu, na wakaamini, kisha wakachamngu na wakafanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mazuri.