قُلْ يَٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَٰبِ لَا تَغْلُوا۟ فِى دِينِكُمْ غَيْرَ ٱلْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوٓا۟ أَهْوَآءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا۟ مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا۟ كَثِيرًا وَضَلُّوا۟ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Wala msifuate matamanio ya kaumu waliokwishapotea tangu zamani, na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Wala msifuate matamanio ya watu walio kwisha potea tangu zamani, na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa.