يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَسْـَٔلُوا۟ عَنْ أَشْيَآءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْـَٔلُوا۟ عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلْقُرْءَانُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا ٱللَّهُ عَنْهَا وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo mkidhihirishiwa, yatawachukiza. Na mkiuliza juu yake wakati inateremshwa Qur-ani, mtadhihirishiwa hayo. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole.