caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ash-Shura, Aya 18

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 62 · 42:18

يَسْتَعْجِلُ بِهَا ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا ٱلْحَقُّ أَلَآ إِنَّ ٱلَّذِينَ يُمَارُونَ فِى ٱلسَّاعَةِ لَفِى ضَلَٰلٍۭ بَعِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wasioiamini huihimiza hiyo Saa ifike upesi, lakini wale wanaoamini wanaiogopa na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanaobishana katika habari za hiyo Saa wamo katika upotovu wa mbali kabisa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWasio amini huihimiza hiyo Saa ifike upesi; lakini wanao amini wanaiogopa, na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanao bishana katika khabari za hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70