caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 6

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:6

وَٱبْتَلُوا۟ ٱلْيَتَٰمَىٰ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغُوا۟ ٱلنِّكَاحَ فَإِنْ ءَانَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَٱدْفَعُوٓا۟ إِلَيْهِمْ أَمْوَٰلَهُمْ وَلَا تَأْكُلُوهَآ إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا۟ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِٱلْمَعْرُوفِ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَٰلَهُمْ فَأَشْهِدُوا۟ عَلَيْهِمْ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wajaribuni mayatima mpaka wanapofikia umri wa kuoa. Mkiona uamuzi wa busara ndani yao, basi wapeni mali zao. Wala msizile kwa kupitiliza na mapema mapema kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na yule ambaye ni tajiri, basi na ajizuilie. Na yule ambaye ni fakiri, basi na ale kwa wema. Na mtakapowapa mali zao, basi washuhudisheni mashahidi juu yao. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70