ٱلَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَٰفِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wanafanya ubahili na wanaamrisha watu ubahili, na wanaficha yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake. Na tuliwaandalia makafiri adhabu ya kudunisha.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAmbao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili, na wanaficha fadhila alizo wapa Mwenyezi Mungu. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya fedheha,