caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 141

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:141

ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓا۟ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَٰفِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوٓا۟ أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ فَٱللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ وَلَن يَجْعَلَ ٱللَّهُ لِلْكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao wanawangojelea. Basi mkipata ushindi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, wao husema: "Kwani hatukuwa pamoja nanyi?" Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda, wao huwaambia: "Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukawakinga kutokana na hawa Waumini?" Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70