وَلَن تَسْتَطِيعُوٓا۟ أَن تَعْدِلُوا۟ بَيْنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ فَلَا تَمِيلُوا۟ كُلَّ ٱلْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلْمُعَلَّقَةِ وَإِن تُصْلِحُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake, hata mkikakamia. Kwa hivyo, msiegemee moja kwa moja mkamwacha (mmoja wao) kama aliyetundikwa. Na mkisikizana na mkamcha Mungu, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.