لَّئِن لَّمْ يَنتَهِ ٱلْمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْمُرْجِفُونَ فِى ٱلْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَآ إِلَّا قَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitina katika Madina hawataacha, basi kwa yakini tutakupa mamlaka juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako isipokuwa muda mchache tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.