فَنَادَتْهُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ وَهُوَ قَآئِمٌ يُصَلِّى فِى ٱلْمِحْرَابِ أَنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًۢا بِكَلِمَةٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, Malaika wakamwita hali ya kuwa amesimama katika chumba akisali kwamba: Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya Yahya, atakayesadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana, na mtawa, na ni Nabii miongoni mwa walio wema.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAlipo kuwa kasimama chumbani akiswali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema.