caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 19

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:19

إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلْإِسْلَٰمُ وَمَا ٱخْتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ وَمَن يَكْفُرْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, Dini kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na hawakuhitilafiana wale waliopewa Kitabu isipokuwa baada ya kujiwa na elimu, kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Na mwenye kuzikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70