caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 15

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:15

قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَٰجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِٱلْعِبَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, niwaambie yaliyo bora kuliko hayo? Kwa waliomcha Mungu kwa Mola wao Mlezi ziko Bustani zipitazo mito chini yake. Watadumu humo, na wake waliotakaswa, na radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona vyema waja wake.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Nikwambieni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wachamngu ziko Bustani kwa Mola wao zipitazo mito kati yake. Watadumu humo, na wake walio takaswa, na wanazo radhi za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70