caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Aal-i-Imraan, Aya 103

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 89 · 3:103

وَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا۟ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَآءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِۦٓ إِخْوَٰنًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msitengane. Na ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu: Mlipokuwa maadui nyinyi kwa nyinyi, naye akaziunganisha nyoyo zenu; na kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa kwenye ukingo wa shimo la Moto, naye akawaokoa kutokana nao. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Ishara zake ili mpate kuongoka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70