caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 284

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:284

لِّلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَإِن تُبْدُوا۟ مَا فِىٓ أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ ٱللَّهُ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi vya Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na mkidhihirisha yaliyo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atawahesabu kwayo. Kisha atamsamehe amtakaye na amwadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniViliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70