caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 275

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:275

ٱلَّذِينَ يَأْكُلُونَ ٱلرِّبَوٰا۟ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِى يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيْطَٰنُ مِنَ ٱلْمَسِّ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْبَيْعُ مِثْلُ ٱلرِّبَوٰا۟ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلْبَيْعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰا۟ فَمَن جَآءَهُۥ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ وَمَنْ عَادَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ أَصْحَٰبُ ٱلنَّارِ هُمْ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wanaokula riba, hawasimami isipokuwa kama anavyosimama aliyezugwa na Shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa walisema: Hakika, biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Basi mwenye kujiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akakomeka, basi yake ni yaliyokwishapita. Na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia, basi hao ndio watu wa Motoni, wao watadumu humo.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70