caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 240

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:240

وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَٰجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَٰجِهِم مَّتَٰعًا إِلَى ٱلْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِى مَا فَعَلْنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanawaacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumbani. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika yale waliyojifanyia wenyewe kwa wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyo jifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70