وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَٰبِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعْدِ إِيمَٰنِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْحَقُّ فَٱعْفُوا۟ وَٱصْفَحُوا۟ حَتَّىٰ يَأْتِىَ ٱللَّهُ بِأَمْرِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanapenda lau wangekurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwishawapambanukia haki. Basi sameheni na tupilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atakapoleta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.